Whitney Houston Akutwa Amefariki Hotelini
Whitney Houston nyota wa muziki wa Marekani alikutwa amefariki dunia kwenye chumba cha hoteli aliyokuwa amefikia kwenye hoteli ya Beverly Hilton Hotel mjini Los Angeles ambako alienda kwaajili ya kuhudhuria party kabla ya kuanza kwa sherehe za tuzo za muziki za Grammy.
Whitney ambaye alitamba sana kwa nyimbo zake zake nyingi za masuala ya mapenzi kama vile "I Will Always Love You" pia alitamba kwenye anga ya filamu kwa filamu zilizotamba sana kama vile The Bodyguard na Waiting to Exhale.
Kipaji chake cha muziki kiliharibiwa na matumizi ya madawa ya kulevya ambayo yalipelekea kuharibika kwa maisha yake na baadae kuvunjika kwa ndoa yake iliyokuwa imejaa matatizo mengi na mumewe Bobby Brown mwaka 2007.
Whitney amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48. Alifariki usiku wa kuamkia leo kwa saa za Tanzania.
Whitney na wapambe wake walichukua karibuni vyumba vyote vya ghorofa ya nne ya hoteli hiyo na walikuwa wakiponda starehe tangu alhamisi.
Whitney ambaye aliuza zaidi ya nakala milioni 55 za nyimbo zake nchini Marekani pekee, alikutwa amefariki kwenye chumba chake hotelini na juhudi za madaktari kuokoa maisha yake ziligonga mwamba.
Mwili wake umehamishwa monchwari kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi wa sababu ya kifo chake ingawa polisi wanasema hadi sasa hakuna dalili ya kufanyika kwa faulo yeyote katika kifo chake.
Post a Comment