Staa mrembo wa Bongo Movies, Irene Paul ameibuka mshindi wa tuzo za
Tanzania Film Awards (TAFA) 2015 kwenye kipengele cha muigizaji bora wa
kike ‘Best Actress (in Lead Role)’ ambapo alikuwa akichuana na Irene
Veda ,Yvonne Cherrie ‘Monalisa’ , Rose Ndauka na Shamsa Ford.
Irene ameeleza kuwa filamu ya Never Give Up aliyoicheza na staa kutoka Ghana Van Vicker ndioiliyomfanya ashind tuzo hiyo.
“Filamu
iliyonifanya niwe msanii bora wa 2015 ni NEVER GIVE UP niliyoitwa na
mzee kambi na niliyocheza na van vicker kutoka ghana van vicker” Ire
alieleza na kuongeza haya kupitia ukurasa wake mtandaoni
“Laiti njia za Mungu zingekuwa za binadamu nahisi basi tungekuwa na
historia tofauti,nasema hivyo maana natafakari nashindwa ila kwa vile
amedhihirisha yupo na hana upendeleo NA AKISEMA NDIO HAKUNA WA
KUPINGA,naongea na wewe kijana mwenye hitaji lako unaloamini ukifanikiwa
utafika mahali fulani,haijalishi ni mda gani,haijalishi machoni pa
wengi ni pagumu kiasi gani kinachojalisha ni nguvu na bidii unayoiweka
katika kuitimiza ndoto yako ndipo patakapomfanya Mungu abariki na kuweka
wepesi wa kupata ndoto yako THIS WAS MY DREAM"
Hongera sana Irene.
Home
»
Gossip News
» Baada ya Kutajwa Kama Muigizaji Bora wa Kike Kwenye Tuzo Za TAFA 2015, Irene Paul Ameyasema Haya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment