Msanii wa filamu nchini, Shamsa Ford amekiri kuwahi kutoka kimapenzi na Nay wa Mitego na baadaye wakaachana.
Shamsha na Nay wa Mitego walikuwa wakizungumza kwa pamoja ndani ya
Global TV hivi karibuni. “Ukweli ni kwamba finally nilikuwa na mahusiano
ya kimapenzi na Emanuel (Nay) lakini tumeachana,” alisema Shamsa.
Kwa upande wake Nay alisema uhusiano ulikuja baada ya kuwa marafiki.
“Tulikuwa washkaji, mahusiano yetu yalianza hivyo,” alisema rapper huyo.
“Tulienda Masaki baada ya kukaa mida fulani wakati wa kuondoka kusema
kweli, kidogo nikaanza kuvutiwa na Shamsa Ford, katika kuagana nikaomba
mimi nikamwambia mimi mwenzako matatizo yangu ni haya.
Bahati nzuri yeye pia hakuwa mzito, nahisi na yeye alikuwa amesoma
kitu kwangu labda ambacho kilimvutia. Tuli-kiss na for the first time
tulikuwa tumeonana siku hiyo na kwamba kila mtu alikuwa tayari kwa
lolote litakalotokea. So tukaanza hivyo, kilichotufanya tuendelee kuwa
connected ni lile kiss la siku ya kwanza,” aliongeza Nay.
Bongo5
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment