MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda amefunguka
kuwa watu wanaomsema vibaya kuhusu yeye kupewa kichapo na mpenzi wake,
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ wanakosea kwani anaamini kufanywa hivyo ni
mahaba.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda akiwa na mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Mziwanda
alisema kuna taarifa zimeenea kuwa huwa anapigwa na Shilole pindi
anapokosea lakini ukweli si kupigwa ‘live’ bali ni kupigwa kimahaba.
“Jamani kupigwa wanakozungumzia watu sielewi lakini mimi ananipiga
kimahaba, wanaosema kuwa mpenzi wangu ananipiga washindwe, watuache kwa
raha zetu,” alisema Shilole.
Post a Comment