Habari ya mjini! Gumzo katika ulimwengu wa mastaa Bongo
ni kitendo cha mkali wa muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ kuendelea kujiachia na staa wa mrembo mwenye maskani yake
nchini Uganda na Afrika Kusini ‘Sauz’, msanii Zarinah Hassan ‘Zari’ au
‘The Boss Lady’ huku aliyekuwa ‘kiburudisho’ wa jamaa huyo, Wema Isaac
Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akijibu mapigo kwa kumnasa mwigizaji Joseph
Van Vicker wa Ghana, Ijumaa lina sarakasi nzima.
Wema Sepetu na Van Vicker wakiwa kwenye pozi.
WEMA ATIMKIA GHANA
Wakati Diamond akitimkia
Marekani kwenda kutumbuiza kwenye sherehe za 53 za Uhuru wa Tanganyika
kwa Wabongo waishio nchini humo (Diaspora), Desemba 9, mwaka huu, Wema
yeye alitimkia kwenye Mji Mkuu wa Ghana jijini Accra kuungana na Van
Vicker kwa ajili ya ‘projekti’ kama ilivyokuwa kwa Diamond na Zari.
Habari za uhakika zilizothibitishwa na Wema mwenyewe zilieleza kwamba
yupo nchini humo kwa ajili ya kurekodi filamu huku wawili hao wakiwa
ndiyo wahusika wakuu.
PICHA ZA MAHABA NIUE
Mapema Jumanne iliyopita,
picha za mahaba niue za mastaa hao zilianza kuvuja kwenye mitandao
mbalimbali ya kijamii huku kila mmoja akimsifia mwenzake kuwa ni mkali.
Wema Sepetu akimkumbatia Van Vicker kwa hisia.
VICKER AMSIFIA WEMA
“Nasisimka na napenda namna
unavyofanya na kuipenda kazi yako. Nafurahi kufanya kazi na wewe,”
aliandika Van Vicker akimsifia Wema ambaye naye alizipokea sifa hizo kwa
mikono yote.
MABUSU
Baadaye waliachia picha nyingine kali zaidi ambazo
ziliwaonesha wawili hao wakiwa kimahaba zaidi ambapo Wema alionekana
akimbusu jamaa huyo kwa hisia kali.
KUMBE WEMA ALIPATA MWALIKO
Habari kutoka kwa
mmoja wa wasimamizi wa Wema aliyeomba hifadhi ya jina zilieleza kwamba,
hivi karibuni mwanadada huyo alipokea mwaliko wa kucheza sinema nchini
Ghana kutoka kwa Van Vicker na wala hakuwa na kipingamizi kwani ni fursa
aliyokuwa akiisubiri kwa muda mrefu.
“Ndiyo imetoka hivyo, sasa hivi ni mwendo wa kimataifa zaidi, hakuna
kulala hadi kieleweke,” alitamba mmoja wa mameneja wa Wema na kuongeza:
“Mpango ulianza tangu kipindi kile Van Vicker alipokuja Bongo kuigiza
na Mzee Chilo (Mohamed Olotu). Kilichokuwa kinasubiriwa ni mipango tu
ikamilike.”
ANAMLIPIZA DIAMOND?
“Hakuna, hayo ni mambo ya
kizamani, mbona ishu ilikuwepo hata kabla ya kummwaga Diamond? Unajua
hizi timu ndiyo zinakuza mambo tu lakini hawayakuzi kwa ubaya, ni namna
walivyo na mapenzi na msanii wao.”
TEAM WEMA VICHEKO
Katika hali ya kushtua, ghafla
wafuasi wa Wema (Team Wema) waliokuwa wamezimwa na wale wa Diamond
(Team Diamond) katika mitandao ya kijamii waliibuka upya.
Safari hii walikuwa wakiachia vicheko na kujisifia kwamba wao ni muziki mnene hivyo hawawezi kushindana na watoto wadogo.
“Huyo bibi bomba (Zari) si lolote. Cheki Madam (Wema) kavuka mipaka
hadi Afrika Magharibi. Mtangoja sana. Sasa ni taifa kwa taifa hadi
kieleweke,” ilisomeka sehemu ya maoni ya Team Wema kwenye Instagram na
kupata dolegumba (likes) nyingi.
Mkali wa muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipozi na Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady.
TEAM DIAMOND NAO
Kwa upande wao, Team Diamond
nao walikuja juu na kuwapa makavu Team Wema kuwa watangoja sana kwani
tayari jamaa siyo wa Afrika tena bali duniani kote.
VAN VICKER NI NANI?
Van Vicker amezaliwa mwaka 1977 ambapo ameoa na amejaliwa kuwa na watoto wanne.
Ni mwigizaji mkubwa barani hasa Afrika Magharibi akiwa amejijengea jina
katika tasnia ya filamu nchini Ghana ya Ghollywood na Nigeria huko
Nollywood akiwa ni mkurugenzi wa kampuni kubwa ya kuzalisha sinema ya
Sky + Orange Productions.
AMEIGIZA SINEMA GANI?
Baadhi ya filamu
alizocheza ni pamoja na Divine Love, Neat Job, Friday Night, The Hands
of Time, One Night in Vegas, Total Love, When One Door Closes, Amina,
Unstopable na nyingine kibao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment