Wema Sepetu: Wimbo wa “Ntampata Wapi”, Diamond Hakuniimbia Mimi
Mrembo na staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu ametoboa kuwa wimbo wa “Ntampata Wapi” ulioimbwa na aliekuwa mpezi wake, Diamond Platnumz hakuimbiwa yeye, hii ni kutokana na watu wengi kudhani kuwa wimbo huu alitungiwa yeye ukizingatia kuwa wakati wimbo huo unatoka ndio kilikuwa kipindi wametoka kuachana.
“Leo nasema rasmi kuwa hii nyimbo hakuniandikia mimi….because nilikuwa naisikia hii nyimbo hata wakati tulipokuwa kwenye uhusiano amekuwa akiimba, akiindika kwahiyo ilikuwa tu ni moja ya nyimbo zake kama anavyoandika nyimbo zote lakini nadhani tu timing ya kutoka ndio kidogo imekuwa na utata because kaitoa timing ambayo watu wote wakadhani kamuimbia Wema but in real sense noo,” aliongeza Wema.
Wema ameyasema hayo hivi majuzi alipokuwa jijini Arusha wakati akifanya mahojiano na kituo cha redio cha Radio 5 cha jijini humo.
Post a Comment