Msanii wa Endless Fame Films, Mirror amesema alimrekodi Nuh Mziwanda
wakati akimtongoza bosi wake Wema Sepetu sababu hakupendezwa na kitendo
hicho alichokiona kama ni utovu wa nidhamu.
Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Mirror
alisema hawezi kufurahi kumuona ‘dogo’ tu akimtongoza bosi wake.
“Mimi sina matatizo na Nuh cha kwanza na sikurekodi kwa nia ya watu
wasikilize,” alisema. “Kwa sababu hata tukiongea ukweli Nuh na madam ni
vitu viwili tofauti, [Wema] ni boss, mkubwa hata kwangu. Mimi nilikuwa
naangalia movies na sikurekodi kwa nia hata kama akija kusikia
girlfriend wake ajue Nuh ndio alikuwa anamsumbua madam,” aliongeza.
“Sijawahi kusikia mtu mwingine akimtongoza madam, siwezi kufurahi Nuh
akimtongoza bosi wangu kwa sababu yeye ni dogo kama mimi, halafu yeye
ana mwanamke wake pia.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment